1.
Kipindi chote cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa amekuwa akijihusisha na uelimishaji na uhamasishaji kupitia
makongamano, warsha za vijana, pia uandishi kupitia Blog yake ya Jielimishe Kwanza! iliyobeba jina la kampuni
iitwayo Jielimishe Kwanza! Social Enterprise yenye makao makuu jijini Dar es salaam, Tanzania.
Kazula amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha mtazamo chanya katika nyanja za ajira, elimu, mazingira na biashara
kupitia makala mbali mbali zilizosheheni ndani ya Blog yake maarufu iliyojinyakulia nafasi ya pili kitaifa kwa mwaka
2013 kama The Best Inspirational Blog in Tanzania.
Hayuko nyuma sana katika kujiendeleza kielimu, mwanzoni mwa mwaka 2014 alianza kufanya shahada ya uzamili
ya Sayansi ya Mazingira yenye vionjo vya Biashara na Ujasiriamali katika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia-
Nelson Mandela, Arusha-Tanzania.
Nikinukuu moja ya sentensi katika mafunzo yake yahusuyo mtazamo anasema;
Mtazamo wako kukuhusu na kuwahusu wengine, unakuwa uhalisia wako kama ukiamini na kujichukulia
Katika kitabu hiki anauliza Mtazamo Wako Ni Upi? Ukizingatia kuwa Mtazamo Wako, Maisha Yako. Ungana naye
hatua kwa hatua kupitia mkusanyiko wa makala zake kuhusu mtazamo ili kutambua mtazamo ulio nao na kuelekea
kuwa na mtazamo chanya ulio na tija ya mafanikio na furaha maishani.
Henry Kazula ni mwanzilishi na mmliki wa kampuni -Jielimishe Kwanza!
Social Enterprise inayojihusisha na kutoa mafunzo ya kushawishi mabadiliko
ya pamoja ndani ya jamii kwa vijana na wadau mbali mbali katika nyanja za
mazingira, elimu, ajira, biashara, ujasiriamali na ujasiriamali jamii.
Pia, Kazula ni mjasiriamali, mwandishi, mwelimishaji jamii, mhamasishaji wa
hadhara na mtaalam wa masuala ya saikolojia ya malezi na mazingira, amekuwa
bega kwa bega katika shughuli mbali mbali za maendeleo ya vijana na jamii
kwa ujumla hasa alipokuwa akishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali
kama; Youth for Africa (YoA) na Global Platform-Actionaid Tanzania yote
ya jijini Dar es salaam katika ujasiriamali na ujasiriamali jamii, pia kuibua
mbinu za pamoja kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana.