Figa la tabia katika elimu ya juu:tufundishe nini, tufundishaje?
1. Figa la tabia katika
elimu ya juu: Tusomeshe
nini, tusomeshaje?
Kassim Hussein, PhD
kassimhussein2002@yahoo.com
Cell: 0754360174
2. Maudhui
Katika mchakato wa kusoma na
kusomesha, sufuria ya ya elimu
huwekwa juu ya mafiga matatu:
Maarifa (knowledge)
Stadi (skills)
Tabia (behaviors)
3. Msukumo
Yako mambo kadhaa yamenipa msukumo:
Kwanza tukiunda mitaala huwa rahisi kuanisha
maarifa na stadi zinazotakiwa kusoma au
kusomesha.
Mathalani:
Tunafahamu kazi za mhasibu na ili mhasibu au
awe na maarifa husika tunaoorodhesha
yanayohitajika. Mitaala yetu hutaja maarifa pia
huoorodhesha vitabu vya kiada na vya kurejelea
kufikia malengo hayo.
4. Msukumo
Kuhusu tabia, mitaala yetu huwa
kimya na hakuna malengo wala,
tabia husika hazijaooridheshwa
na hakuna hata vitabu vya kiada
au machapisho ya kurejelea.
5. Msukumo
Katika kuanzisha mwaka mpya wa
masomo na hata wakati wa
mahafali, wageni rasmi husisitiza
tabia njema kwa wanafunzi au
wahitimu. Aghlabu tabia zenyewe
huwa haziwekwi wazi.
6. Msukumo
Niliombwa na wenzagu
niwape nasaha na uzoefu
wangu, nikawa sina. Ila nikatoa
ahadi na leo ninatimiza kwa
maswali mawili.
7. Msukumo
Maswali ni juu ya tabia:
tusomeshe nini na tusomesheje?
Maswali ambayo nikaona
yanahitaji kuanzisha mjadala juu
ya tabia ili kuyatafutia majibu
9. Msukumo
Ilikuwa haja yangu kujaribu tafiti
shirikishi kuhusu jambo la msingi
katika elimu ya Tanzania.
Hivi ni nini kimefanya wanafunzi
kuandika matusi au bongo flavour
katika mitihani?
10. Msukumo
Ni nini kinafanya wahitimu
wengine wapendelewe katika
soko la ajira ?
11. Tabia - maana
Ni sehemu ya elimu iliokamilika au
UWEZO
Inahusika na tathmini ya utu, vitu,
mambo au matukio
Inaelekeza fikira (cognitive function)
Inashawishi hisia (affective function)
Inaathiri hatua (conative function)
12. Wengine
huiona TABIA USAWA WA BAHARI
Wengine
hawaioni
MIKO VIGEZO UAMUZI
Mtazamo
DHAMIRA MAADILI - IMANI
Organizational Behavior 12
13. Nadharia ya tabia
Hulka ambazo mtu huzaliwa nazo.
Vipaumbele juu ya kufikiri, kutoa
maamuzi, mahusiano na nishati ya mwili.
Kuna tabia zitokanazo na malezi, upendo
na mazingira ya mtu kutokana na wazazi
na jamii aliyokulia.
Kuna tabia zianzofunzwa sambamba na
taaaluma yaani kuzisoma na kusomesha.
14. Asiefunzwa na ,
hufunzwa na .
Katika nadharia ya tatu, juu
ya tabia katika mchakato
wa elimu ya juu, kuna
orodha ndefu ya tabia
stahiki.
15. Asiefunzwa na .., hufunzwa na .
Tabia zote ni muhimu, ila kwa
wahadhiri kuna haja ya
kuziainisha, na kuamua
kuziiingiza baadhi kwenye
mitaala rasmi au iliokubalika
na wengi.
16. Kuna haja, ulazima wowote?
Chimbuko la haja: hutokana na
wasomi wenyewe; yaani
msomaji na msomeshaji
Wadau wengine: taasisi,
serikali, jamii nk
17. Kuna haja?
Dunia ni soko la ajira inahitaji wahitimu
walioelimika yaani wenye uwezo (maarifa
+ stadi + tabia)
Uwezo ( au competency) ni jumuisho la
maarifa (applied), stadi za kazi na tabia
(attributes/ behaviours/attitudes) ili
kufanya kazi nzuri zaidi ya kiwango cha
kawaida. (McClelland, 1973)
18. Haja za Wasomi
Kuna nadharia moja ya
muundo, tabia na utendaji
(S C P) kwamba utendaji
wa mtu unaathriwa na
tabia na inatokana na
muundo.
19. Haja za Wasomi
Muundo huenda ukawa umiliki,
vyanzo vya mapato, kipimo
(ukubwa), jiografia, wakati , jinsia nk
hulazimisha kusoma au kusomesha
tabia fulani.
Mathlani kuhusu umiliki: kuna vyuo
vya serikali , vya dini au vya binafsi?
20. Mifano vyuo vya dini
Vyuo vya taasisi za dini hutaka
kutambuliwa kuwepo kwa mungu,
kujenga tabia za dini husika na
hairuhusu kufuru kwa mfano dhana
za Charles Darwin kuhusu asili ya
binadamu.
21. Mifano vyuo vya dini
Vyuo hivi hufundisha tabia
zinazo endana na imani za dini
kama vile haramu, halali ,
makuruhu, utumishi wa
mungu nk
22. Mifano vyuo vya dini
Kwa mfumo huu, chuo ni zizi, walimu
na wachungaji na wanafunzi ni
wachungwa. Kwa hiyo wachungaji ni
masuuli wataulizwa mbele ya
mungu juu ya dhima ya tabia za
waliowachunga kama zimeenda
kombo
23. Mifano: Vyuo vya serikali
Vyuo vya serikali hustawisha fikra ya kutafuta
ukweli na kuruhusu imani mbalilmbali na hata
zile zinazo kubali kuwepo kwa mungu na zile
zinazokataa kuwepo kwa mungu.
Wakati wa kupigania uhuru, au wa ukombozi
vyuo hivi hukazania fikra za walioshika uongozi
wa serikali.
Mathlani serikali ya kijamaa ilizaa watu wenye
tabia za uzalendo, wapenda haki na utu na
haya yalikuwepo ndani ya mitaala.
24. Vyuo binafsi
wadhamini huwa na malengo ya kufikia
ndoto za walengwa na hulenga
kufanikiwa, kushinda, na ujasiria mali.
Tabia zinazowekwa makazo ni pamoja na
kuwa mshindani, mjasiriamali, kiongozi
nk
25. Vyuo binafsi
Sera za vyuo zimeelemea kuwa
mwanafunzi ni mteja na mteja
anahaki ya kuchagua
atakachotaka kusoma au
kusomeshwa.
26. Vyuo binafsi
Msomeshaji anawajibu wa
kumridhisha kila mteja, mara ya
kwanza na kila mara. Elimu ni bidhaa
na kwa hiyo mfumo wa masomo ni
wasoko huria.
27. Vyuo binafsi
Mwanafunzi huamua atakacho soma
yeye na msomeshaji atalazimika
kumridhia mteja wake. Kwa maana
hii, tabia hata figa la tabia katika
elimu ni uchaguzi wa msomi
mwenyewe.
28. Vyuo binafsi
Tabia nazo huwa katika bidhaa kama
vile Entrepreneurship, Diversity, nk.
Wasomeshaji/ wahadhiri hufanikiwa
kama wanasajili wanafunzi wengi na
kutathminiwa kuwa wanawajali na
kuwaridhisha wateja wao.
29. Swali letu la msingi
Tufundishe nini, tufundishaje?
kuandaliwa orodha ya tabia
muhimu zinazostahiki kila mhitimu
awe nazo
Tuainishe zile za muhimu,
Tuzifundishe vipi?
30. Jitihada za kuanisha Tabia
Azimio la UNESCO juu ya tabia ni pamoja
na uraia, tabia za kushirikiana na jamii,
uwezo, kuchunga haki za binadamu,
maendeleo endelevu, demokrasia, na
amani katika misingi ya haki.
Nyingine ni utamaduni wa kujiendeleza
na kuleta maendeleo
31. Jitihada za kuanisha tabia JKN
(Elimu ya Kujitegemea)
Mwalim alibainisha tabia za kujitegemea,
tabia za kuhudumia umma na tabia za kutatua
au kuwaondelea watu (wananchi) matatizo na
migogoro.
Ameainisha:
Ushirikiano ( na sio maendeleo ya mtu binafsi)
Fikra za usawa
Wajibu wa kutoa huduma
32. Jitihada za kuanisha tabia JKN
(Elimu ya Kujitegemea)
Akili ya kuchunguza
Uwezo wa kujifunza
Uwezo wa kukataa au kukubali vitu
wanavyofanya wengine kufuatana na mahitaji
binafsi
Kujiamini kama mtu sawa na huru
Anaethamini wengine na anathaminiwa kwa
anachokifanya na si anachokipata
33. Jitihada za kuanisha
SAUT- To prepare and mould men and
women of integrity, devotion, commitment,
principled, accountable, capable of taking risk;
for future performance of leadership roles in
society, and occupying positions of influence in
public life, professions, industry and commerce
in order to be able to realize the ideals of a
good and just society
34. Jitihada za kuanisha
SAUT. In other words to have
personnel who are mentally and
morally fit. ... to us, through the
Word of God, Catholic Tradition and
Teaching of the Church
35. MUM works to produce highly educated and well trained human
resources inculcated with the appropriate aptitudes and attitudes for
the material, moral and spiritual development of the society through:
Community Built Academic
Knowledge on Respect and freedom,
Seeking Tolerance Creativity and
Innovation
Collegiality and Spiritual and
Integrity and Collaboration Academic
Prudence Balance
Responsibility Trust and
Excellence and Teamwork
Accountability
36. Serikali katika OPRAS inataka tabia hizi
1. Kufanya kazi katika timu 13. Kuridhisha unachohitajika kutimiza
2. Kuwezana na wafanyakazi 14. Kufanya kazi za ziada
wengine 15. Kukubali majukumu na kuyatimiza
3. Kuheshimika na wengine 16. Kufanya maamuzi sahihi
4. Kujieleza kimaandishi 17. Kuwahudumia wateja
5. Kujieleza kwa kusema 18. Kuonyesha unafuata na wasaidiza
6. Usiikvu na kuelewa wako
7. Kujifunza na kuwafundisha 19. Kuwasaidia viongozi wako
unaowasimamia 20. Utii wa maelekezo halali ya viongozi
8. Kupangana kupangilia wako
9. Kuongoza, kuhamasisha na 21. Kutumia muda wa kazi kufanya
kutatua migogoro mambo ya kazi
10.Kuanzisha na ubunifu 22. Kutoa huduma bora bila ya kichocheo
11.Kuwasilisha kazi sahihi kwa chochote
wakati
12.Bidii na kutochoka
37. Tufundishe Utu
Utu au kwa lugha za kusini ubuntu ni
ufundi au tasnia ya a kuwa binadamu
(Ivorgba, 2009).
Utu au ubuntu kwa semi za Zulu:
umuntu ngumuntu ngabantu,
inamaanisha utu wa mtu unapatikana
toka kwa mtu mwingine
38. Tufundishaje?
Kwanza: Tukumbuke kuwa
huwezi kufundisha usichokijua
au kuwa nacho!!
Haja ya kujiandaa/kuandaliwa
kuwa na tabia husika.
39. Tufundishaje?
Pili, maandalizi ni pamoja na njia za
kufundisha, kupima na kutathmini tabia
Tatu, kuikimu nidhamu na kuiweka hali shwari
ya kusoma na kusomesha. Kowalski, (2003)
anatoa mifano ya tabia za kitoto, za kuudhi na
inajumuisha kuchelewa, kuundoka kabla ya
wakati, kuongea pembeni, kuchelewesha kazi,
udanganyifu, kujipatia alama zisizo haki.
40. Tufundishaje?
Boice (1998) anaona tabia hizi
pia huchangiwa na
wasomeshaji kwa kutoweka
misingi ya nidhamu na
kuisimamia.
41. Tufundishaje?
Tabia za kuharibu uendeshaji wa
masomo, usumbufu, kuwapunguzia
wasomaji wengine ari na kuwavunjia
heshima.
Tunasimamia vipi nidhamu?
43. Tufundishaje?
Kuweka masomo maalumu yenye kufundisha
tabia husika
Baadhi ya tabia ziwe ni sehemu ya masomo
mengine
Njia za kuwasilisha somo juu ya tabia zitokane
na utaalamu wa msomeshaji na ari ya
msomaji
44. Hitimisho
Haja ya kuzitambua tabia husika
Kuziweka katika mitaala
Kuwaandaa walimu kuzisomesha
Kuwaandaa wanafunzi kujifunza
45. Marejeo
Boice, R. (1998). "Classroom incivilities." In K. A. Feldman &
M. B. Paulson (Eds.), Teaching and learning in the college
classroom (2nd ed.) (347-369). Needham Heights, MA:
Simon & Schuster Custom Pub
Kowalski, R. M. (2003). Complaining, teasing, and other
annoying behaviours. New Haven, CT: Yale University Press.
Ivorgba, E.A. (2009) Values in African thought.
(http://valuesinworldthought.authorfriendly.com/pages/p....)
McClelland, D. (1973). Testing for competence rather than
for "intelligence." American Psychologist, 28, 1-14
McClelland, D. (1978) Guide to Behavioral Event
Interviewing, Boston: McBer and Company.
46. Marejeo
Nyerere, J. Elimu na Kujitegemea, Oxford
University Press
Nyerere, J. Uhuru na Maendeleo. Oxford
University Press 1968
UNESCO. 1998. The Role of Higher Education
in Society: Quality and Pertinence. Paris,
UNESCO.
URT, OPRAS form