1. USHINDI KATIKA UJANA
Kijana ni nani?
Kijana ni mtu wa kike au wa kiume mwenye umri kati ya miaka 15
na 45.
Biblia inasema nini juu ya kijana?
Biblia imenena mambo mengi juu ya kijana, na baadhi ya hayo ni
kuwa fahari ya kijana ipo katika nguvu zake (Mithali 20:29).
Kijana ana nguvu nyingi, neno la Mungu linakaa ndani yake na
kisha amemshinda shetani(1Yohana 2:14b).
Yohana anawaandikia vijana akisema wana nguvu nyingi, pili neno
la Mungu linakaa ndani yao na kisha wamemshinda shetani. Nguvu
yaweza kuwa ya kiroho au ya kimwili, maana zote ni za muhimu
na mara nyingine hutegemeana katika utendaji.
Nguvu moja ikikosekana hujitokeza upungufu unaoweza
kupelekea uharibifu kama vile mtu kurudi nyuma kwa sababu ya
majaribu. Nguvu ya kimwili ya mtu wa Mungu ikitumika kwa
mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu, yaweza kupelekea mtu
kuwa na nguvu ya kiroho iletayo ushindi juu ya hila na mitego ya
2. yule mwovu.Hapa ina maana kuwa, kwa mtu wa Mungu ukiwa na
nguvu ya kimwili na unaongozwa na Roho wa Mungu utamtumikia
Mungu pasipo ulegevu, tofauti na mzee ambaye anaweza kuhitaji
kufanya jambo lakini nguvu ya kwenda kufanya hana, hilo nalo
Mhubiri aliliona na kumhamasisha kijana kutumika akiwa bado
anazo nguvu. Mhubiri12:1 Mkumbuke Muumba wako siku za
ujana wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya Yohana
anawaandikia vijana akionyesha sifa za aina ya vijana aliokuwa
akiwalenga. Anatazamia kwamba kijana akiitumia nguvu hiyo
kama ilivyokusudiwa na Mungu, na kulisoma neno, kuomba kwa
bidii zake zote, matokeo yake atakuwa na hazina tele ya neno
ndani mwake, na kisha atamshinda shetani, maana anazo nguvu
za kiroho na za kimwili. Kijana wa aina hii hana hofu maana hata
shetani akija kwa sura gani au akitumia mazingira gani, haogopi
maana silaha alizo nazo (Neno) ni tishio kwa adui. Mungu
anawatafuta vijana kama hao wabebao silaha hiyo ya Bwana ,
nyakati zote, kila mahali na kwa bidii. ..Nimewaandikia ninyi
vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani
yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu(I Yohana 2:14b).
3. Biblia inasema kijana akilitii Neno la Mungu na kulifuata
litasafisha njia yake. Litamkamilisha kwa kiwango anachotaka
Mungu, kwa makusudi ya Mungu na kwa utukufu wa Mungu.
Kwahiyo ili kijana aweze kuishi maisha matakatifu, yenye ushindi
tele na yanayomtukuza Mungu yampasa kuisafisha njia yake kwa
kutii, akilifuata neno la Mungu. Zab.119.9Jinsi gani kijana
aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
Kijana, kufanikiwa kuisafisha njia yako kutategemeana na wewe
mwenyewe utakavyotumia nguvu zako. Yakupasa kuelekeza nguvu
zako katika maombi, kujisomea Neno la Mungu, hii ni pamoja na
kulitafakari na kulitendea kazi. Kwa kufanya hivyo utapata
nafasi nzuri ya kumsikiliza Mungu na kujua ni nini mpango na
makusudi yake kwako. Kijana hupaswi kulala usingizi tangu jioni
hadi asubuhi na tangu January hadi Desemba, huo ni msiba wa
kutosha kwa kijana maana Biblia inasema mtu wa aina hiyo
atapata umaskini wa kumtosha. Si vema kijana kuzagaa, ukikutwa
na adui ukiwa umezagaa atakutumikisha katika matakwa yake. Ni
muhimu sana kijana kuwa na mikakati na kuiombea ili kupata
uongozi wa Roho Mtakatifu. Mungu anajali sana kijana kuwa na
4. mkakati. Mfano mzuri ni namna alivyomwandaa Yoshua kushika
nafasi ya Musa. Awali ya yote alimhakikishia uwepo wake pamoja
na kijana huyo, na akamwahidi kutomwacha wala kumpungukia
kabisa: Hapatakuwa mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele
yako siku zote za maisha yakositakupungukia wala sitakuacha.
(Yoshua 1. 5).
Hapa Mungu anamhakikishia Yoshua kuwa, hata kutokee tatizo
kubwa kiasi gani, hata vitisho viwe vikubwa namna gani, hata
ainuke nani, asingeweza kuzuia wala kukwamisha kusudi la Mungu
katika huduma aliyokuwa anakabidhiwa na Mungu, ya kuwafikisha
Waisraeli nchi ya Kanaani. Hali kadhalika wewe kijana, yumkini
bado unawategemea wazazi au ndugu, lakini kwakuwa umeokoka
labda wamekutenga, hawataki kukupa huduma, hata masomoni
unatishiwa kufukuzwa kwasababu huna karo; yumkini umeoa au
umeolewa na huyo mume au mkeo anakutesa kwa ajili ya wokovu;
kazini unanyanyaswa na mkubwa wako wa kazi au wafanyakazi
wenzio, halikadhalika kwenye biashara zako wanakutesa kwa njia
mbalimbali. Katika hali yoyote ile, jambo la muhimu uwe na
uhakika kwamba Mungu yupo pamoja na wewe na kwamba
5. hatakuacha wala hatakupungukia. Hivyo usikate tamaa, azimia
kutomwacha Mungu kabisa, simama katika haki na ahadi za
Mungu, utaona ushindi mkubwa.
Baada ya Mungu kutoa uhakika juu ya uwepo wake kwa kijana
huyo Yoshua, alimpa mikakati ya namna atakavyoweza kufikia
lengo ambalo lilikuwa kuwafikisha Waisraeli katika nchi ya ahadi,
Kanaani. Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi.
Mungu hapendezwi na uvivu, alitaka Yoshua awe hodari tu na
ushujaa mwingi na siyo mtu wa kujihurumia hurumia bali awe
mwepesi wa kwenda anakotakiwa, kutekeleza majukumu ambayo
Mungu angempa inavyotakiwa, kwa wakati unaotakiwa, na pasipo
hofu. Huo ndiyo ushujaa.
2. ...uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru
Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume au wa
kushoto.(Yosh. 1.7).
Mungu anamwambia Yoshua, aangalie kutenda sawasawa na
sheria yote aliyokuwa ameamriwa na Musa mtumishi wake
6. Mungu. Swala kuu hapa ni utii wa neno la Mungu. Kwamba kijana
hatarajiwi kuwa msikilizaji tu wa Neno la Mungu na kuendelea na
maisha ya kidunia. Kijana anahitajika kuwa msikiaji na
mtendaji/mtekelezaji wa maagizo ya Mungu ndani ya Neno.
Mungu anasisitiza katika mstari wa nane kuhusu kutafakari
Neno. Mungu alimtaka Yoshua, kuhakikisha siku zote za maisha
yake anafanya Neno la Mungu kuwa sehemu ya maisha yake.
Alimtaka akiwaza awaze (atafakari) Neno mchana na usiku,
maongezi yake yawe na msingi katika Neno. Kuhusu kutendea
kazi Neno, Mungu alimwambia Yoshua aangalie kutenda
sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo (ndani ya
torati/Neno.
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali
yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia
kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa
humo."(Yoshua 1:8).
Kwa maana hiyo, iwe usiku iwe mchana kijana saa zote unatakiwa
kutafakari neno la Mungu siyo kuwaza shida, taabu na
7. masumbufu ya dunia hii. Kulitafakari Neno huja baada ya
kulisoma, Daudi alisema: Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
nisije nikakutenda dhambi (Zab. 119.11).
Alilisoma na kisha akalihifadhi moyoni. Neno hilo katika hazina
ya moyoni, likawa mshauri, mwongozo na faraja wakati wa
majaribu, mapito au mateso. Na kwa kulitamka likafanyika fimbo
ya kumwangamiza adui, na kufungua milango ya baraka
iliyofungwa na adui na pia likatumika hata kubadilisha mazingira
kama Ezekia alivyotamka uhai kwa mifupa, ikainuka ikiwa hai na
kuwa kikundi kikubwa cha watu.
Ili uwe na maisha yenye mwelekeo wa ki-Mungu na ya mfano,
epuka kabisa kuwaza mambo mapotofu, epuka mazungumzo mafu
yasiyo na uhai wa ki-Mungu maana yatakuharibu wewe pamoja na
wakusikilizao, pia matendo yoyote yaliyo kinyume na Neno la
Mungu epukana nayo. Mungu alijua kuwa kijana huyu Yoshua
asiposisitiziwa na Mungu mwenyewe, asipoishi kwa Neno ambalo
ndiyo lishe bora ya roho yake, angeharibikiwa, na hapo kusudi la
Mungu la ukombozi wa wana wa Israel lingeyumba. Hali kadhalika
wewe usipoishi kwa kulitii Neno na kufanya kama linavyokuagiza,
8. adui atayumbisha mpango wa Mungu katika maisha yako,
matokeo yake ni kuchanganyikiwa, kukata tamaa na hata kufa
kabisa kiroho. Lakini ukisimama pasipo kujali mazingira
yanayokuzunguuka, Mungu anao mpango mzuri sana na maisha
yako na ndiyo maana amekuokoa (amekuita). Yumkini wewe ndiye
wa kwanza kumpa Yesu maisha yako katika familia au ukoo wako.
Mungu anategemea kukutumia wewe kulifikisha kundi hilo nchi
ya ahadi kama alivyomtumia Yoshua. Zoezi hilo litafanikiwa iwapo
utakuwa hodari tu na mwenye ushujaa mwingi, na kutenda
sawasawa na Neno kama linavyoletwa kwako na Roho Mtakatifu
mwenyewe kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujumbe huu
unaousoma sasa.MUNGU akubariki sana