3. Mkusanyaji na Mwandishi: SELEMAN ABDALLAH;
ISLAMIC HELP TANZANIA- 2012-03-06
Email: tanzania@islamichelp.org.uk, /
kakasule2@gmail.com
Phone: +255689131400 or 0754 371115
4. UTANGULIZI
DHANA YA UWEZESHAJI KIUCHUMI
DHANA YA UJASIRIA MALI
Dhana ya ujumla ya ujasiriamali:
Sehemu ya Pili: Mjasiriamali
HAJA YA UJASIRIAMALI: Kwanini tunahitaji
kuusoma Ujasiriamali?
UMUHIMU WA UJASIRIAMALI.
Dhana ya biashara
UISLAMU NA BIASHARA
FAIDA ZA BIASHARA.
ADABU ZA BIASHARA KIISLAMU
5. USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA BIASHARA
MPANGO WA BIASHARA NA MRADI
ANDIKO LA MRADI (Project Proposal)
MPANGILIO WA BIASHARA (Business Plan)
MPANGO WA MASOKO (Market Plan)
UTUNZAJI KUMBUKUMBU KATIKA BIASHARA
UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU
UMAKINI KATIKA GHARAMA ZA BIASHARA
CHANGAMOTO ZA BIASHARA.
MBINU ZA BIASHARA
BIASAHARA NA FAMILIA:
6. UTANGULIZI
Uchumi ni sekta ambayo huchochea kwa
namna moja au nyingine maendeleo ya
mwanaadamu
Biashara ni moja ya sehemu kuu ya
uchumi na maiongiliano makuu ya uchumi
hupatikana kwa kupitia biashara,miradi na
kwa ujumla Ujasiriamali.
Kufanya ujasiriamali ni moja katika njia za
kujipatia kipato na jitihada ilizungumzwa
na dini
7. Kujipatia riziki ya halali ni jambo
linalomfurahisha sana Mola na hili
limedhihirishwa katika hadithi na
mafundisho ya mtume (saw), hadithi
iliyopokelewa na At-twabaraniy: -
inayosema Kutafuta chumo la halali ni
Wajibu kwa kila muislamu
8. Kwa kuzingatia haya pamoja na uhitaji wa
dhana hii kuna changamoto juu ya
ufahamu na ujuzi maalumu juu ya
Biashara, miradi na ujasiriamali katika
ujumla wake.
Ujasiriamali ni ujuzi kama zilivyo tasnia
nyingine, lazima usomwe na kufunzwa kila
anayetaka ufanisi wake na matunda yake.
9. Dhana inayojengeka miongoni mwa jamii
kuwa ujasiriamali ni swala la kipaji cha
kuzaliwa nacho, kurithi au kujulikana pasi na
elimu ni dhana potofu inayowakwamisha
wale wanaotaka kuchukua hatua kuufanyia
kazi ujasiriamali.
Mjasirimali mmoja anasema maneno yafuatayo:
Mengi katika usikiayo kuhusu ujasiriamali sio
sahihi. Si uchawi; si mazingaombwe; na hauna
lihusianalo na maumbile, ni nidhamu na, kama
nidhamu nyingine, Inawezekana kwa kusomwa.
Peter F. Drucker
10. DHANA YA UWEZESHAJI
KIUCHUMI
Katika maisha yeyote ya wanaadamu uchumi ni
sehemu kubwa ya maisha yao kwa kuwapatia njia
na fursa za maisha.
Dhana hii ni mahimu kufanyiwa jitihada na njia za
kuikwamua ili kuleta tija na muonekano wa ubora
katika ngazi ya jamii.
Kujikwamua kiuchumi ni hatua ya kufanya jitihada
na michakato mbalimbali ili kuboresha mapato na
kuinua ufanisi wa matokeo yanayotazamiwa
kutokana na uchumi.
11. Sehemu kubwa ya ufanisi katika
mchakato wa kujikwamua na kujikomboa
kichumi unapatika kwa jamii kujihusisha
na mpango wa Ujasiriamali.
Ujasiriamali husaidia kipato cha
mwanajamii na kutoa mchango mkubwa
katika sehemu au mahali anapopatikana.
13. Sehemu ya Kwanza:
Maana ya Ujasiriamali:
Ujasiriamali:
Ni utekelezaji au utendaji ambao mtu
anapanga, anafanya, anasimamia na
kuendesha na kukisia mashaka au hatari
kwa kuthubutu kufanya jambo la kiuchumi
au kijamii ua biashara.
14. Maana ya Ujasiriamali
Neno ujasiriamali linatokana na maneno
mawili ambayo ni UJASIRI na MALI. Hivyo
maana ya ujasiriamali ni kuwa na: -
Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata
mali;
Uwezo wa kutambua fursa za biashara
haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa
hizo pindi zinapojitokeza; na
Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo
vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za
biashara.
15. Ujasiriamali: ni utashi juu ya kufanya kitu;
ni njia ya kufikiria, kufikia na kufanya
jambo au kitu fulani.
Ujasiriamali ni mchakato ambapo mtu
anachukua hatua kutumia fursa bila kujali
hali ya rasilimali alizonazo
16. Ni mchakato ambapo mtu anafanisi, kusimamia,
kuandaa na kuratibu ubunifu, uboreshaji na uvumbuzi,
kujenga thamani na uthamini unaompa faida au kutoa
manufaa na kuzingatia na kujenga ukuaji na upekee wa
tahmani kwa jamii inayomzunguka
MCHAKATO
Upekee Mjasiriamali
UBUNIFU
Kukua
Kujenga Kuunda kundi/
Faida Taasisi
Kujenga
Thamani
17. Sehemu ya Pili: Mjasiriamali
Mtu ambaye anathubutu kufanya, Jambo,
vitendo au mradi wenye manufaa.
Aliyechochewa au mwenye vichocheo vya
kuendelea kiuchumi kwa kutafuta na kubuni
njia mpya za kujikwamua na kufanya
mambo.
Mjasiriamali kwa tafsiri ya Drucker, ni
ahamishae rasilimali kutoka eneo lenye
uzalishaji mdogo na kupeleka katika eneo
lenye uzalishaji mkubwa na mavuno (mengi).
18. HAJA YA UJASIRIAMALI:
Malengo ya Kujifunza:
Kuweza kuanzisha na kumiliki kitega
uchumi: Hapa kitega uchumi (enterprise)
inamaanisha swala lolote la kiuchumi au
kijamii aidha biashara au mradi wa faida.
Kusaka fursa za kijamii: Ujasiriamali
unajenga ushawishi wa kuyabadili
matatizo kuwa fursa hasa katika jamii.
19. Malengo ya Kujifunza:
Uelewa na uhabarisho wakibiashara: Kuelewa
biashara katika maono mapana,
Kuabadili utashi wakimaisha ndani ya kazi na
ajira: Hutoa moyo wa utegemezi binafsi/ uhuru
kwa kupitia kujijenga uwezo.
Ajira Binafsi: Kwa kupitia ujasiriamali ni rahisi
kupata ajira na kujisimamia mwenyewe.
Ubora wa maisha: Kuanzisha biashara kunampa
fursa muasisi kuwa na baadhi ya uchaguzi juu ya
lini, wapi,na nani, na vipi ufanye kazi.
21. Faida za kuwa Majsiriamali
Husaidia kubadili fikra za vijana, utashi na
mtazamo juu ya uzoefu wa jamii au hali ya
kazi za jamii kama masoko, maradhi, na
maswala ya ajira.
Husaidia utambuzi binafsi na kukuza akili.
Huchochea kutumia rasilimali kwa
ukamilifu na fursa zinazopatika katika jamii
na mzingira yetu.
22. Faida .
Ujasiriamali ni alama ya maendeleo ya miradi
na umakini, kujituma na mafanikio katika
biashara
Mapinduzi ya ujasiriamali ni chachu ya ukuaji
wa uchumi na maendeleo.
Ujasiriamali huweza kuathiri hali yetu ya
baadae kwa njia nyingi kama:
Kuboresha ubunifu wa fursa : Mafano Simu
ndogo rahisi kubeba zilizounganishwa na faksi na
Komputa ndogo aina za Laptop huweza kubadili
gari, treni, au mapokezi ya ndege kuwa ofisi.:
23. Dhana ya biashara-Business
Biashara ni matendo ambayo
humuhusisha mtu katika kununua na
kuuza huduma au bidhaa kwa lengo la
kupata faida.
Biashara ni pamoja na hali ya kununua na
kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalamu,
wito na makubaliano ya kipekee yenye
lengo la kibiashara kwa nia ya kupata
faida.
24. Mambo ya kuzingatia katika
uazishaji wa biashara:
Katika kuamua aina ya biashara unayotaka
kufanya tafadhali zingatia vigezo vifuatavyo,
Namna ya upatikanaji wa bidhaa hiyo au
huduma unayoitarajia kuiuza au kuitoa.
Idadi ya washindani wanaouza ama kuitoa
bidhaa hiyo.
Matakwa ya wateja katika eneo husika na
idadi yao.
Gharama za uendeshaji wa biashara husika.
25. Mambo ya kuzingatia
Taratibu mbalimbali za ulipaji ada na kodi
mbalimbali.
Hali ya hewa ya eneo husika.
Hali halisi katika eneo la biashara, angalia
mwenendo wa maisha ya wakazi katika
eneo husika mfano, amani na utulivu, vita,
mfumuko wa bei, n.k.
26. MJASIRIAMALI NA
MFANYABIASHARA
Ni ukweli ulio wazi kuwa si kila
anayeuza au mfanyabiashara ndogo
ndogo ni mjasiriamali.
Imekuwa ni 'fashion' kwa sasa nchini
tangu nchi ijiunge katika mfumo
unoangozwa na soko kwa kila muuzaji
wa bidhaa na mtoaji wa huduma kujiita
mjasiriamali.
27. Kwa ufupi mjasiriamali ni mtu yeyote ambaye
haogopi kuweka mipango na kushindwa,
tofauti na mfanyabiashara yeye huwa na
mtazamo wa kuwekeza kwa ajili ya faida
pekee.
Mjasiriamali mhimili wake mkuu ni ubunifu
Kuzalishwa wa bidhaa mpya, njia mpya za
uzalishaji kugunduliwa, kutafutwa kawa masoko
mapya na utumiaji wa rasilimali
zinazomzunguka.
28. Misingi ya Ujasiriamali
1. Elimu juu ya ujasiriamali na kujifunza;
ni muhimu kwa kila anayejihusisha na
dhana ya ujasiriamali akaujua ujasiriamali
na sikuchukulia kuwa ni jambo ala kuiga
ama kunakili kutoka kwa watu
waliofanikiwa au wanaojihusisha na
ujasiriamali, kujifunza huku kuwe kwa
nadharia na vitendo.
2. Ubunifu na uvumbuzi: Majasiramali
haswa ni yule anaeyekuwa na kubuni
vyanzo na mbinu mbalimbali za
kuboresha utendaji wake
29. 3. Kukua na kupanuka: ni muhimu
mjasiriamali akue na kutanuka kimaslahi na
si kuwa katika hali moja tua kila mara,
anapaswa kutanuka kimtaji,kiutendaji na
kimahusiano, hili huboresha huduma na
uwanda wake wa malengo. Hivyo ni muhimu
pia majaisiriamali kuwa mtu wa mipango na
kuwa na uelekeo Fulani anaotakaa kufikia
sehemu Fulani.
4. Kujaribu na kudhamiria: Mjasiiramali si mtu
wakuaogopa kutenda apindia aionapoa fursa
na kuitathmini kuwa ianpaswa kuendewa.
Hivyo si muoga katika kujaribu
30. Maeneo ya kutengeneza mtandao
wako kama mjasiriamali;
Washindani wako:
Biashara ni ushindani lakini sio uadui.Kama
unataka kuwa mjasiriamali mwenye
mafanikio ni vizuri sana ukawajua
washindani wako wa kibiashara.
Mshindani wako anaweza kukufaa pia.
Anaweza kuzidiwa na kazi akakusukumia
zingine.Jitambulishe,jenga uhusiano mzuri wa
kibiashara.
31. Vyombo vya Habari:
Kama mjasiriamali,ni muhimu ukajuana na
watu wanaoendesha au hata kumiliki
vyombo hivi vya habari.
Na zaidi angalia vile ambavyo vipo karibu
zaidi na eneo lako la ujasiriamali.
Kutangaza na kupata taarifa.
32. Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO):
Mjasiriamali makini ni yule ambaye
anadhamiria kuisaidia jamii yake kwa njia
moja au nyingine
Isitoshe jamii iliyo bora,iwe kiafya,kielimu
nk ni wateja wako wazuri wa siku za
mbeleni.
34. Hujihusisha na ujasiriamali tu
Ni mtu anayejihusisha na Biashara Ndogo
tu
Ni mtu asiye na Elimu
Ni kamari na kubahatisha
Ujasiriamali unazaliwa nao
Inahitaji mawazo makubwa
Ni kazi rahisi