2. Yaliyomo
Sera ya maji 1991
Mapitio ya sera ya maji ya 1991
Sera ya maji ya mwaka 2002
Malengo ya sera
Muundo wa sera
Huduma za maji vijijini
Masuala ya kisera
Watekelezaji wa sera ni nani
3. Sera ya Maji ya 1991
Sera ya kwanza ya maji Tanzania
Lengo: Maji safi na salama kwa wote ifikapo 2002
Serikali ndio mwekezaji, mwendeshaji na msimamizi
wa miradi na mtunzaji wa rasilimali
4. Mapitio ya Sera ya Maji 1991
Yalianza mwaka 1996
Sababu Mapungufu ya sera ya 1991
Hali halisi ya upatikanaji maji na uendelevu
50% wanapata maji, 30% vituo vya maji havifanyi kazi
Kutoshirikisha kikamilifu wadau hususan wananchi
Kutoipa umuhimu sekta binafsi ktk utoaji huduma
Mapungufu katika mfumo wa kitaasisi na kisheria
5. Sera ya Maji ya 2002
Imetokana na mapitio ya sera ya mwaka 1991
Imeandaliwa kushirikisha wadau wote muhimu
Imeundwa kuzingatia malengo ya dira ya taifa 2025 na
MKUKUTA
Imeweka mfumo madhubuti na endelevu wa
kusimamia rasilimali za maji
Pia taratibu za kisheria na muundo wa kitaasisi wa
kutekeleza sera
6. Malengo ya Sera
Kushirikisha walengwa kubuni, kupanga, kujenga,
kuendesha, kufanya matengenezo na kuchangia
gharama za huduma
Utunzaji na usimamizi endelevu wa rasilimali za maji
kwa kushirikisha wadau wote
Kupunguza majukumu ya utekelezaji kwa serikali ili
kusimamia, kuratibu, kushauri, kuwezesha na kutoa
miongozo
7. Muundo wa Sera
Sera ina sehemu kuu tatu
i. Usimamizi wa rasilimali za maji
- kuweka na kuendeleza mfumo endelevu na madhubuti wa
kusimamia rasilimali maji
ii. Utoaji wa huduma ya maji vijijini
- Kuboresha afya za wananchi wa vijijini, kuchangia
kupunguza umasikini kwa kutoa huduma endelevu ya
maji safi, salama na ya kutosha
iii. Utoaji wa huduma ya majisafi na majitaka mijini
- Kuweka mfumo endelevu wa kutoa huduma kwa bei nafuu ili
makundi yote yafaidike
9. Madhumuni
Upatikanaji wa huduma endelevu kwa gharama iliyo ndani ya uwezo
wa wananchi vijijini.
Kuweka bayana majukumu na wajibu wa wadau mbalimbali.
Kuweka mkazo wananchi kulipia sehemu ya gharama za ujenzi wa
miradi, gharama zote za uendeshaji na matengenezo ya miradi yao
Kubadili utaratibu ili wananchi wabuni, waanzishe na kuendesha
miradi yao wenyewe.
Kuhamasisha Sekta Binafsi kushiriki katika kugharamia, kujenga,
kuendesha na kutoa huduma ya maji vijijini.
Kuboresha afya ya jamii kwa kuunganisha mipango ya utoaji wa
huduma ya maji, usafi wa mazingira na elimu ya afya.
10. Misingi ya Sera
Maji ni hitaji la msingi na haki ya kila mtu
Matumizi ya maji kwa ajili ya binadamu ni muhimu
kwanza
Maeneo yenye uhaba kupewa kipaumbele cha miradi
Maji ni bidhaa ya kiuchumi
Kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji
Huduma endelevu
11. Masuala ya kisera
Ushiriki wa jamii
Kumiliki miradi ya maji, kuchagua teknolojia, kubuni,
usanifu, ujenzi wa miradi, uendeshaji na matengenezo
ya miradi
Kushirikisha sekta binafsi kutoa huduma ya maji
vijijini
Serikali kuwa mdhibiti, mwezeshaji na mratibu wa
maji vijijini
Jinsia zote kushiriki kikamilifu katika miradi ya maji
12. Masuala ya kisera....
Kiwango cha chini cha utoaji huduma vijijini
Lita 25 za maji safi na salama kwa mtu kwa siku
Vituo vya maji viwe umbali usiozidi mita 400
Kila kituo kuhudumia watu 250
Udhibiti wa utoaji huduma za maji vijijini
Wananchi kugharamia miradi ya maji vijijini
Wananchi kuendesha miradi yao ya maji kisheria
Kuwa na mfumo mzuri wa ufuatiliaji na tathmini ya
miradi ya maji
14. Ni nani watekelezaji wa sera ya
maji?
1. Wananchi
Ndio watekelezaji wakuu. Wanapaswa
Kubuni, kumiliki, kusimamia na kuiendesha miradi yao ya maji.
Kulipia gharama za uendeshaji, matengenezo, ukarabati na upanuzi
wa miradiya maji
Kulinda vyanzo vya maji na maeneo yanayozunguka vyanzo hivyo.
Kuhakikisha kuwa kuna uwiano mzuri kati ya teknolojia
iliyochaguliwa na kiwango cha huduma na upatikanaji wa maji kwa
upande mmoja, na uwezo wa kiuchumi wa watumiaji maji wenyewe
kwa upande mwingine.
Kutambua kuwa wanawake ni miongoni mwa wahusika wakuu
katika utoaji wa huduma ya maji vijijini.
16. Ni nani watekelezaji wa sera ya maji.......
2. Serikali za Mitaa
Jukumu kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya
maji safi na salama.
Hivyo ni wasimamizi na wawezeshaji wa jamii. Majukumu
yao ni;
Kusimamia na kufuatilia upatikanaji wa maji.
Kusimamia vyombo vya watumia maji na kuhakikisha jamii
inakusanya fedha kwa ajili ya marekebisho ya miradi ya maji
Kuhakikisha miundombinu ya maji inalindwa, na kufanyiwa
matengenezo
Kutoa msaada wa kitaalamu tatizo linapotokea
Kuwezesha wanajamii kupata vipuri pale ambapo vinahitajika
18. Ni nani watekelezaji wa sera ya maji?....
3. Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Ni wasimamizi wakuu wa sera
Majukumu yao ni
kuandaa sera na mipango
kuratibu, kusimamia na kutoa miongozo
kuziwezesha halmashauri za wilaya, kukagua na
kutathimini utekelezaji wa miradi ya maji
19. Ni nani watekelezaji wa sera ya maji?.....
4. Mashirika binafsi na Vyombo vya habari
Kuhakikisha sera zinawanufaisha wananchi
Kusambaza taarifa za kisera, mipango na bajeti
Kutoa elimu kwa umma
Kuhamasisha ushiriki wa wananchi
Kuwajengea uwezo wananchi ili;
Kushiriki katika utekelezaji wa sera
Kufuatilia utekelezaji wa sera
Kutathmini utekelezaji wa sera