1. WADUDU na MAGONJWA
SUGU kwa KILIMO CHA
KAHAWA NA UDHIBITI WAKE
Happy Sikalengo
Bwana Shamba – NAFCO Mbozi
happy.Sikalengo@yahoo.com +255 755 325 442
3. Utangulizi
• Kahawa hupandwa katika
nchi zaidi ya 50 duniani
kote.
• Brazil ni mzalishaji
mkubwa wa kahawa
duniani, hadi magunia
milioni 25 (60kg) mwaka
2003.
• Ambayo ilichangia kwa
zaidi ya 30% ya kahawa
yote ulimwengu
4. Utangulizi
• Ni zao la kudumu, hadi
miaka 50.
• Kahawa ni zao kubwa la
biashara linaloliingizia
taifa fedha nyingi za
kigeni.
• Zao hili linakabiliwa na
changamoto nyingi.
9. RUHUKA - Coffee Berry Borer
• The beetle Hypothenemus
hampei
• Ruhuka hutoboa tundu moja
au zaidi kupitia kwenye kovu
la ua la tunda la kahawa.
• Wana asili ya afrika lakini
waesambaa duniani kote.
10. RUHUKA - Coffee Berry Borer
• Vizazi vya ruhuka huendelezwa na
matunda yanayobakia juu ya
mibuni na yale yanayodondokea
chini.
• Pia majike yanaweza kujilisha
kwenye matunda machanga.
• Ruhuka jike hutaga mayai 30 - 60
katika kipindi cha majuma 3 - 7.
11. RUHUKA - Coffee Berry Borer
UDHIBITI
• Ondoa matunda yote yaliyobaki
juu ya mibuni, na okota
yaliyodondoka shambani mara
baada ya kuvuna.
• Chunguza kuwepo kwa ruhuka
(Juni, Julai). Akiwepo nyunyizia
sumu za asili kama mwarobaini,
utupa.
• Chuma mara kwa mara (kila siku
14) ili kahawa isikaukie juu ya mti.
12. RUHUKA - Coffee Berry Borer
Kutumia viatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
NB: Sumu zitafanya kazi ya kudhibiti kabla ruhuka hajaingia ndani
ya punje (majuma 16 kabla ya kuvuna).
13. BUNGUA MWEUPE WA SHINA
Coffee Stem Borer
• Monochamus leuconotus
• Bungua mweupe huishi kwenye
kahawa aina ya arabika. Pia
huishi kwenye miti jamii ya
mibuni.
• Kusini mwa afrika, hasara ya
hadi 25%, mashambulizi ya
Zaidi ya 80% vimeripotiwa.
14. BUNGUA MWEUPE WA KAHAWA
White Coffee Stem Borer
• Hutaga mayai 23.
• Mayai hutagwa/pachikwa chini ya
magamba ya mibuni nusu meta juu
ya usawa wa ardhi.
• Huanguliwa na kutokea bungua
mweupe baada ya siku 21.
• Bungua mweupe hutafuna mti
kuelekea ndani na kufanya
uharibifu kwa miezi 20 kabla ya
kuwa buu.
• Buu hubadilika kuwa mdudu kamili
baada ya miezi 2 - 4 akiwa ndani ya
shina / mti.
15. Kudhibiti Bungua Mweupe
Njia za kawaida
• Ng’oa na choma mibuni iliyoshambuliwa sana.
• Baada ya mavuno kwangua / sugua mashina ya kahawa
kuondoa magamba kwa gunzi ili kuondoa mayai na
maeneo ya kutaga.
• Kagua shamba na kukusanya mbawa kavu wa bungua
weupe na kuwaua. (kuanzia mwezi Oktoba, Novemba,
Disemba, Januari).
• Ua bungua weupe kwa kuwaondoa kwa waya (Oktoba /
Novemba; Aprili, Mei).
• Weka mafuta ya wanyama kwenye matundu kuvutia
sisimizi watakao wala bungua.
16. Kudhibiti Bungua Mweupe
Kutumia viatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
17. VIDUGAMBA - Green Scales
• Hawa ni wadudu walio na umbo
bapa la mviringo na hukaa
mahali pamoja.
• Hufyonza damu ya mmea na
hutoa sumu inayoharibu majani
ya kahawa.
• Mara nyingi masizi honekana
kwenye majani na matawi na
misafara ya sisimizi huelekea
mahali walipo ili kujipatia asali
wanayozalisha.
18. VIDUGAMBA -
Green Scales
• Jike hutaga hadi mayai 500
chini ya mwili wake.
• Ndani ya masaa machache
mayai huanguliwa.
• Vitoto hivi vina uwezo wa
kusafiri kutoka mmea mmoja
hadi mwingine kwa urahisi.
• Ndio chanzo cha kusambaa
wadudu.
19. VIDUGAMBA - Green Scales
Kutumia viatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
Agromethrin 10EC
Agrothrin
100-120ml 10ml 7 days
20. VIDUNGATA –
Coffee Root Mealybug
• Wadudu hawa huonekana kama
unga mweupe kwenye matawi
machanga , maua na matunda.
• Wadudu hawa wanaweza
kutembea umbali kidogo
ingawaje huonekana kama
wamegandia sehemu moja.
21. Coffee Root Mealybug
Maisha na Uharibifu
• Katika hatua za kukua, vidungata
watoto hufanana na wale wapevu na
ndizo hatua zinazofyonza
virutubisho vya mmea. Mti wenye
ushambulizi hudhoofika na baadaye
hufa.
• Misafara ya sisimizi hufuata makao
ya vidungata kwa ajili ya asali
wanayozalisha.
22. Udhibiti
Njia za kawaida:
• Kilimo sango (all cultural practices) kizingatiwe
hususani ukataji matawi; kusugua mashina ya
kahawa.
• Kuhimiza wadudu marafiki ambao mara nyingi
huwala au kutaga mayai ndani yao.
• Kuzuia sisimizi wasiwafikie walipo kwa kupaka shina
mikorogo ya sumu za asili kama utupa
24. VITHIRIPI - Coffee thrips
• Wadudu hawa ni wadogo sana;
wanalo umbo la kuchongoka na
hawaonekani kwa urahisi.
• Mkulima anaweza kuwatambua kwa
kuona dalili za mashambulizi yake
upande wa chini wa majani ya
kahawa ambayo huwa na mng’ao wa
rangi ya fedha (Silvery).
• Pia vitone vyeusi husambaa kwenye
majani yaliyoadhirika.
• Dalili hizi pia huonekana kwenye
punje na majani machanga.
25. VITHIRIPI - Coffee thrips
UDHIBITI
• Kilimo Sango:-
- Matumizi ya matandazo
- Kusugua mashina ya kahawa
- Kukwatua shamba
• Matumizi ya Asili:-
- Tumbaku - tumia kilo 1
tumbaku / lita 15 za maji
- Utupa - tumia gm 750 / lita 15
za maji
26. VITHIRIPI - Coffee thrips
Kutumia viuatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
Agromethrin 10EC
Agrothrin
100-120ml 10ml 7 days
27. Kidomozi (Leafminer)
• Kidomozi ni kiwavi ambaye
ametokana na kuanguliwa kwa
mayai ya jamii ya nondo mdogo
(mm 3 - 4) mweupe ambaye
mchana hujificha chini ya majani ya
kahawa na kuruka usiku.
• Kama mti ukitikiswa nondo hawa
huruka kwa muda mfupi na kisha
kujificha tena.
28. Kidomozi (Leafminer)
• Kidomozi hutaga mayai madogo yenye rangi ya kung’aa, juu ya
majani
ya kahawa.
• Mayai haya huonekana kama yamepangwa kwenye safu na
wakati mwingine huwa kwenye vifurushi.
• Viwavi ni weupe na wadogo (mm 6 - 8) na mara
wanapoanguliwa hupenya ndani ya jani, chini ya ngozi ya juu.
• Hula kwa kutengeneza mitaro, myembamba kwenye jani zima,
ambalo baadaye hufa na kuanguka.
• Kidomozi anakaa ndani ya jani kwa muda wa wiki (5) tano na
baadaye hugeuka kuwa buu ambaye anaweza kujitundika kwa
uzi wa utando kwenye jani au huanguka chini.
29. • Udhibiti:
• Kilimo Sango:-
• Usafi wa shamba, kukata matawi, kukwatua shamba na
matandazo.
• Sumu ya asili:-
- Mkojo wa Ng’ombe 1:4
- Utupa - angalia vithiripi
- Tumbaku
31. MINYOO YA MIZIZI
Nematodes of Coffee
• Minyoo huingia katika mizizi na
kusababisha mizizi kuwa na
vinundu.
• Mimea hudumaa, majani ya
njano na kushindwa kukua.
32. MINYOO WA MIZIZI –
Nematodes of Coffee
Udhibiti
• Unga wa mwarobaini
katika kitalu.
• Kabla ya kupandikiza,
hakikisha miche haina
wadudu.
33. MINYOO WA MIZIZI –
Nematodes of Coffee
Kutumia viuatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml
35. Kutu ya Majani –
Leaf Rust
•Kutu ya majani ni ugonjwa
unaoathiri majani ya kahawa
hasa kanda za chini na kati.
•Ugonjwa huu unaathiri kahawa
aina zote; Robusta na Arabika.
•Kutu ya mjani isipodhibitiwa
inaweza kupunguza mavuno kwa
asilimia 60.
36. Madhara yake
•Kutu ya majani hupunguza eneo
la jani la kutengeneza chakula.
• Punje ndogo
• Majani kupukutika
•Ugonjwa ukishamiri hukausha
matawi, shina zima na hatimaye
mti mzima kufa.
37. Kudhibiti
• Tumia red copper kiasi cha kilo 3.8
kwa hekta.
• Tumia Meronil 720 EC (55 ml/15 lt
of water)
• Tumia Agromenol 250 EC (40ml/15
lt of water)
• Njia zingine
• Punguza kivuli kuzunguka mti
wa kahawa.
• Pogolea machipukizi na matawi
katika mti wa kahawa.
38. Chulebuni
Coffee Berry Disease
• Huenea kwa kasi.
• Mbuni ulioshambuliwa haufi ila
mkulima anaweza kupoteza
mpaka 90% ya mavuno kama
hatazingatia namna bora ya
kuuzuia.
• CBD huathiri matunda ya
kahawa hasa kanda za juu na
kati.
• Ushambuliaji ni mkubwa zaidi
wakati wa masika kwani CBD
hupenda hali ya unyevu na hali
ya baridi.
39. Madhara
• CBD hushambulia mibuni katika
hatua tatu muhimu ambazo ni:
. Maua yanapochanua.
. Punje zikiwa changa na laini.
. Punje zinazoiva.
• Maua/matunda
yaliyoshambuliwa hunyauka na
kuanguka.
• Matunda yaliyoiva hukaukia
kwenye matawi na huvunwa
kama buni.
40. Kudhibiti
• Piga Red copper, 4 kg kwa hekta.
• Tumia Meronil 720 EC (55 ml/15 lt ya maji) ndani ya
wiki tatu kabla ya mvua za msimu kuanza.
• Njia zingine
• Punguza kivuli shambani.
• Kata matawi kwa wakati na sahihi.
• Ondoa maotea mara kwa mara.
• Ondoa masalia ya buni zilizoathirika na teketeza kwa
moto.
• Hamasisha majirani kuzuia chulebuni kwa wakati mmoja.
41. MNYAUKO FUSARI
Coffee Wilt Disease
• Hushambulia mashina,
machipukizi na hata punje.
• Ugonjwa wa hushamiri
kwenye mashamba ambayo
hayatunzwi vizuri.
• Viini vya ugonjwa huu
vinauwezo mdogo sana wa
kushambulia mkahawa
wenye afya nzuri.
43. Kudhibiti
• Tumia Meronil 720 EC (55 ml/15 lt za maji).
NJIA ZINGINE
• Palizi ni muhimu kwenye shamba.
• Ukataji sahihi wa matawi.
• Matumizi ya mbolea kwa kiwango kinachoshauriwa.
• Ng’oa na choma moto mikahawa iliyokufa.
• Iwapo ni matawi yanayoonyesha dalili za ugonjwa
matawi hayo yakatwe na kuchomwa moto.
44. MADOA YA KAHAWIA
Brown Eye Spot Disease
• Majani hutoboka.
• Sehemu inayotrngeza chakula
cha mmea hupungua.
• Mavuno hupungua
45. Kudhibiti
• Pulizia copper mapema
kabla ugonjwa kushamiri.
• Tumia Meronil 720 EC (55
ml/15 lt za maji)
Brown Eye Spot
Coffee Bark Disease
48. Kudhibiti Magugu
Magugu Njia za kuyadhibiti
Ndago Ndago Agrosate 250mls/20lts za maji
Nyasi Ulezi Agrosate,
Meraxone 200mls/20lts za maji
Kwekwe Agrosate 250mls/20lts za maji
Majani
mapana
Tambazi,
Mchicha
Meraxone, Agrosate
Vichaka Agrosate 250mls/20lts za maji
50. Namna ya kuongeza ufanisi wa viua magugu
• Magugu yawe yanakua vizuri yasiwe
yameathirika na stress kama ukame, maji
yaliyotuama n.k.
• Nyunyiza magugu yakiwa machanga
• Unahitaji kiasi cha saa 8 baada ya kunyunyiza
bila mvua kunyesha.
• Usinyunyize wakati wa jua kali sana
• Weka kiasi kilichopendekezwa cha dawa
• Tumia kipenyo (nazeli) stahiki.