3. Utangulizi
Kahawa hupandwa katika
nchi zaidi ya 50 duniani
kote.
Brazil ni mzalishaji
mkubwa wa kahawa
duniani, hadi magunia
milioni 25 (60kg) mwaka
2003.
Ambayo ilichangia kwa
zaidi ya 30% ya kahawa
yote ulimwengu
4. Utangulizi
Ni zao la kudumu, hadi
miaka 50.
Kahawa ni zao kubwa la
biashara linaloliingizia
taifa fedha nyingi za
kigeni.
Zao hili linakabiliwa na
changamoto nyingi.
9. RUHUKA - Coffee Berry Borer
The beetle Hypothenemus
hampei
Ruhuka hutoboa tundu moja
au zaidi kupitia kwenye kovu
la ua la tunda la kahawa.
Wana asili ya afrika lakini
waesambaa duniani kote.
10. RUHUKA - Coffee Berry Borer
Vizazi vya ruhuka huendelezwa na
matunda yanayobakia juu ya
mibuni na yale yanayodondokea
chini.
Pia majike yanaweza kujilisha
kwenye matunda machanga.
Ruhuka jike hutaga mayai 30 - 60
katika kipindi cha majuma 3 - 7.
11. RUHUKA - Coffee Berry Borer
UDHIBITI
Ondoa matunda yote yaliyobaki
juu ya mibuni, na okota
yaliyodondoka shambani mara
baada ya kuvuna.
Chunguza kuwepo kwa ruhuka
(Juni, Julai). Akiwepo nyunyizia
sumu za asili kama mwarobaini,
utupa.
Chuma mara kwa mara (kila siku
14) ili kahawa isikaukie juu ya mti.
12. RUHUKA - Coffee Berry Borer
Kutumia viatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
NB: Sumu zitafanya kazi ya kudhibiti kabla ruhuka hajaingia ndani
ya punje (majuma 16 kabla ya kuvuna).
13. BUNGUA MWEUPE WA SHINA
Coffee Stem Borer
Monochamus leuconotus
Bungua mweupe huishi kwenye
kahawa aina ya arabika. Pia
huishi kwenye miti jamii ya
mibuni.
Kusini mwa afrika, hasara ya
hadi 25%, mashambulizi ya
Zaidi ya 80% vimeripotiwa.
14. BUNGUA MWEUPE WA KAHAWA
White Coffee Stem Borer
Hutaga mayai 23.
Mayai hutagwa/pachikwa chini ya
magamba ya mibuni nusu meta juu
ya usawa wa ardhi.
Huanguliwa na kutokea bungua
mweupe baada ya siku 21.
Bungua mweupe hutafuna mti
kuelekea ndani na kufanya
uharibifu kwa miezi 20 kabla ya
kuwa buu.
Buu hubadilika kuwa mdudu kamili
baada ya miezi 2 - 4 akiwa ndani ya
shina / mti.
15. Kudhibiti Bungua Mweupe
Njia za kawaida
Ngoa na choma mibuni iliyoshambuliwa sana.
Baada ya mavuno kwangua / sugua mashina ya kahawa
kuondoa magamba kwa gunzi ili kuondoa mayai na
maeneo ya kutaga.
Kagua shamba na kukusanya mbawa kavu wa bungua
weupe na kuwaua. (kuanzia mwezi Oktoba, Novemba,
Disemba, Januari).
Ua bungua weupe kwa kuwaondoa kwa waya (Oktoba /
Novemba; Aprili, Mei).
Weka mafuta ya wanyama kwenye matundu kuvutia
sisimizi watakao wala bungua.
16. Kudhibiti Bungua Mweupe
Kutumia viatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
17. VIDUGAMBA - Green Scales
Hawa ni wadudu walio na umbo
bapa la mviringo na hukaa
mahali pamoja.
Hufyonza damu ya mmea na
hutoa sumu inayoharibu majani
ya kahawa.
Mara nyingi masizi honekana
kwenye majani na matawi na
misafara ya sisimizi huelekea
mahali walipo ili kujipatia asali
wanayozalisha.
18. VIDUGAMBA -
Green Scales
Jike hutaga hadi mayai 500
chini ya mwili wake.
Ndani ya masaa machache
mayai huanguliwa.
Vitoto hivi vina uwezo wa
kusafiri kutoka mmea mmoja
hadi mwingine kwa urahisi.
Ndio chanzo cha kusambaa
wadudu.
19. VIDUGAMBA - Green Scales
Kutumia viatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
Agromethrin 10EC
Agrothrin
100-120ml 10ml 7 days
20. VIDUNGATA
Coffee Root Mealybug
Wadudu hawa huonekana kama
unga mweupe kwenye matawi
machanga , maua na matunda.
Wadudu hawa wanaweza
kutembea umbali kidogo
ingawaje huonekana kama
wamegandia sehemu moja.
21. Coffee Root Mealybug
Maisha na Uharibifu
Katika hatua za kukua, vidungata
watoto hufanana na wale wapevu na
ndizo hatua zinazofyonza
virutubisho vya mmea. Mti wenye
ushambulizi hudhoofika na baadaye
hufa.
Misafara ya sisimizi hufuata makao
ya vidungata kwa ajili ya asali
wanayozalisha.
22. Udhibiti
Njia za kawaida:
Kilimo sango (all cultural practices) kizingatiwe
hususani ukataji matawi; kusugua mashina ya
kahawa.
Kuhimiza wadudu marafiki ambao mara nyingi
huwala au kutaga mayai ndani yao.
Kuzuia sisimizi wasiwafikie walipo kwa kupaka shina
mikorogo ya sumu za asili kama utupa
24. VITHIRIPI - Coffee thrips
Wadudu hawa ni wadogo sana;
wanalo umbo la kuchongoka na
hawaonekani kwa urahisi.
Mkulima anaweza kuwatambua kwa
kuona dalili za mashambulizi yake
upande wa chini wa majani ya
kahawa ambayo huwa na mngao wa
rangi ya fedha (Silvery).
Pia vitone vyeusi husambaa kwenye
majani yaliyoadhirika.
Dalili hizi pia huonekana kwenye
punje na majani machanga.
25. VITHIRIPI - Coffee thrips
UDHIBITI
Kilimo Sango:-
- Matumizi ya matandazo
- Kusugua mashina ya kahawa
- Kukwatua shamba
Matumizi ya Asili:-
- Tumbaku - tumia kilo 1
tumbaku / lita 15 za maji
- Utupa - tumia gm 750 / lita 15
za maji
26. VITHIRIPI - Coffee thrips
Kutumia viuatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Agrofecron 720 EC 800 ml 50 ml 14 days
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml 7-14 days
Agromethrin 10EC
Agrothrin
100-120ml 10ml 7 days
27. Kidomozi (Leafminer)
Kidomozi ni kiwavi ambaye
ametokana na kuanguliwa kwa
mayai ya jamii ya nondo mdogo
(mm 3 - 4) mweupe ambaye
mchana hujificha chini ya majani ya
kahawa na kuruka usiku.
Kama mti ukitikiswa nondo hawa
huruka kwa muda mfupi na kisha
kujificha tena.
28. Kidomozi (Leafminer)
Kidomozi hutaga mayai madogo yenye rangi ya kungaa, juu ya
majani
ya kahawa.
Mayai haya huonekana kama yamepangwa kwenye safu na
wakati mwingine huwa kwenye vifurushi.
Viwavi ni weupe na wadogo (mm 6 - 8) na mara
wanapoanguliwa hupenya ndani ya jani, chini ya ngozi ya juu.
Hula kwa kutengeneza mitaro, myembamba kwenye jani zima,
ambalo baadaye hufa na kuanguka.
Kidomozi anakaa ndani ya jani kwa muda wa wiki (5) tano na
baadaye hugeuka kuwa buu ambaye anaweza kujitundika kwa
uzi wa utando kwenye jani au huanguka chini.
29. Udhibiti:
Kilimo Sango:-
Usafi wa shamba, kukata matawi, kukwatua shamba na
matandazo.
Sumu ya asili:-
- Mkojo wa Ngombe 1:4
- Utupa - angalia vithiripi
- Tumbaku
31. MINYOO YA MIZIZI
Nematodes of Coffee
Minyoo huingia katika mizizi na
kusababisha mizizi kuwa na
vinundu.
Mimea hudumaa, majani ya
njano na kushindwa kukua.
32. MINYOO WA MIZIZI
Nematodes of Coffee
Udhibiti
Unga wa mwarobaini
katika kitalu.
Kabla ya kupandikiza,
hakikisha miche haina
wadudu.
33. MINYOO WA MIZIZI
Nematodes of Coffee
Kutumia viuatilifu
Pesticide
Dose
PHIPer ha 16 lt tank
Protrin 60 EC 400-800 ml 16 ml
35. Kutu ya Majani
Leaf Rust
Kutu ya majani ni ugonjwa
unaoathiri majani ya kahawa
hasa kanda za chini na kati.
Ugonjwa huu unaathiri kahawa
aina zote; Robusta na Arabika.
Kutu ya mjani isipodhibitiwa
inaweza kupunguza mavuno kwa
asilimia 60.
36. Madhara yake
Kutu ya majani hupunguza eneo
la jani la kutengeneza chakula.
Punje ndogo
Majani kupukutika
Ugonjwa ukishamiri hukausha
matawi, shina zima na hatimaye
mti mzima kufa.
37. Kudhibiti
Tumia red copper kiasi cha kilo 3.8
kwa hekta.
Tumia Meronil 720 EC (55 ml/15 lt
of water)
Tumia Agromenol 250 EC (40ml/15
lt of water)
Njia zingine
Punguza kivuli kuzunguka mti
wa kahawa.
Pogolea machipukizi na matawi
katika mti wa kahawa.
38. Chulebuni
Coffee Berry Disease
Huenea kwa kasi.
Mbuni ulioshambuliwa haufi ila
mkulima anaweza kupoteza
mpaka 90% ya mavuno kama
hatazingatia namna bora ya
kuuzuia.
CBD huathiri matunda ya
kahawa hasa kanda za juu na
kati.
Ushambuliaji ni mkubwa zaidi
wakati wa masika kwani CBD
hupenda hali ya unyevu na hali
ya baridi.
39. Madhara
CBD hushambulia mibuni katika
hatua tatu muhimu ambazo ni:
. Maua yanapochanua.
. Punje zikiwa changa na laini.
. Punje zinazoiva.
Maua/matunda
yaliyoshambuliwa hunyauka na
kuanguka.
Matunda yaliyoiva hukaukia
kwenye matawi na huvunwa
kama buni.
40. Kudhibiti
Piga Red copper, 4 kg kwa hekta.
Tumia Meronil 720 EC (55 ml/15 lt ya maji) ndani ya
wiki tatu kabla ya mvua za msimu kuanza.
Njia zingine
Punguza kivuli shambani.
Kata matawi kwa wakati na sahihi.
Ondoa maotea mara kwa mara.
Ondoa masalia ya buni zilizoathirika na teketeza kwa
moto.
Hamasisha majirani kuzuia chulebuni kwa wakati mmoja.
41. MNYAUKO FUSARI
Coffee Wilt Disease
Hushambulia mashina,
machipukizi na hata punje.
Ugonjwa wa hushamiri
kwenye mashamba ambayo
hayatunzwi vizuri.
Viini vya ugonjwa huu
vinauwezo mdogo sana wa
kushambulia mkahawa
wenye afya nzuri.
43. Kudhibiti
Tumia Meronil 720 EC (55 ml/15 lt za maji).
NJIA ZINGINE
Palizi ni muhimu kwenye shamba.
Ukataji sahihi wa matawi.
Matumizi ya mbolea kwa kiwango kinachoshauriwa.
Ngoa na choma moto mikahawa iliyokufa.
Iwapo ni matawi yanayoonyesha dalili za ugonjwa
matawi hayo yakatwe na kuchomwa moto.
44. MADOA YA KAHAWIA
Brown Eye Spot Disease
Majani hutoboka.
Sehemu inayotrngeza chakula
cha mmea hupungua.
Mavuno hupungua
45. Kudhibiti
Pulizia copper mapema
kabla ugonjwa kushamiri.
Tumia Meronil 720 EC (55
ml/15 lt za maji)
Brown Eye Spot
Coffee Bark Disease
48. Kudhibiti Magugu
Magugu Njia za kuyadhibiti
Ndago Ndago Agrosate 250mls/20lts za maji
Nyasi Ulezi Agrosate,
Meraxone 200mls/20lts za maji
Kwekwe Agrosate 250mls/20lts za maji
Majani
mapana
Tambazi,
Mchicha
Meraxone, Agrosate
Vichaka Agrosate 250mls/20lts za maji
50. Namna ya kuongeza ufanisi wa viua magugu
Magugu yawe yanakua vizuri yasiwe
yameathirika na stress kama ukame, maji
yaliyotuama n.k.
Nyunyiza magugu yakiwa machanga
Unahitaji kiasi cha saa 8 baada ya kunyunyiza
bila mvua kunyesha.
Usinyunyize wakati wa jua kali sana
Weka kiasi kilichopendekezwa cha dawa
Tumia kipenyo (nazeli) stahiki.
Editor's Notes
#5: Asili:
Kahawa ni zao la kudumu ambalo likitunzwa vizuri linaweza kukaa
shambani zaidi ya miaka 50 likiendelea kuvunwa. Asili yake ni kwenye
misitu ya Ethiopia. Iliingizwa Africa mashariki kwenye karne ya 19
na Wamisionari.
Aina:
Kuna aina kuu mbili zinazolimwa Tanzania nazo ni:
1. Arabika
2. Robusta
#10: Ruhuka (Coffee Berry Borer)
Hypothenemus hampei
Ruhuka huishi kwenye mibuni na jamii zake pamoja na mimea jamii
ya mikunde. Ruhuka hushambulia zaidi mibuni aina ya Robusta na
Arabika kwenye ukanda wa chini.
22 TANZANIAN-GERMAN IPM PROJECT
Uharibifu
Ruhuka hutoboa tundu moja au zaidi kupitia kwenye kovu la ua la
tunda la kahawa. Tundu hili huonekana kwenye matunda mabichi au
yaliyoiva. Punje zilizoshambuliwa hubadilika rangi na kuwa kijani cha
bluu. Viwavi wa ukubwa mbalimbali huwepo ndani ya punje. Wingi wao
huweza kufikia 20 kwa tunda. Uharibifu hufanywa na viwavi na ruhuka
wapevu ndani ya punje. Matundu yaliyotobolewa huweza kuwa njia ya
kupenyeza ukungu na bacteria. (Tazama picha Na. 2 Uk 42).
Maisha ya Ruhuka
Jamii ya ruhuka huzaa majike mengi; uwiano wa majike 10 kwa dume 1
yenye uwezo wa kuruka kutoka mti hadi mti. Madume hayaruki hubaki
ndani ya punje yakiendeleza uzao kwa majike wakitoboa matunda na
kutaga mayai ndani ya punje za kahawa.
Vizazi vya ruhuka huendelezwa na matunda yanayobakia juu ya
mibuni na yale yanayodondokea chini. Pia majike yanaweza kujilisha
kwenye matunda machanga.
Ruhuka jike hutaga mayai 30 - 60 katika kipindi cha majuma 3 - 7.
Mayai hutagwa kwa awamu. Kila awamu mayai 12. Huanguliwa baada
ya siku 8. Viwavi wanaotokea hujilisha ndani ya punje. Viwavi wa
hatua mbalimbali za ukuaji huwepo ndani ya punje. Viwavi hujilisha
kwa siku 15 - 19 kabla ya kuwa buu. Buu hubadilika kuwa dudu mzima
(Ruhuka) baada ya siku 7.
Kudhibiti Ruhuka
1. Ondoa matunda yote yaliyobaki juu ya mibuni, na okota yaliyodondoka
shambani mara baada ya kuvuna. Chimba shimo na
ufukie matunda hayo. Kwa kufanya hivi kunakatisha mzunguko
wa maisha ya mdudu huyo.
2. Chunguza kuwepo kwa ruhuka (Juni, Julai). Akiwepo nyunyizia
sumu za asili kama mwarobaini, utupa.
KILIMO BORA CHA KAHAWA 23
Uchunguzi ukionyesha kuzidi kuwepo kwa ruhuka nyunyizia sumu
za viwandani kama; Thiodan 35 au Dursban 48 EC.
3. Weka matandazo ili kuendeleza wadudu marafiki wanao kula
ruhuka. Pia matandazo huozesha matunda yaliyodondoka chini.
4. Kata matawi mara kwa mara.
5. Chuma mara kwa mara (kila siku 14) ili kahawa isikaukie juu
ya mti.
NB: Sumu zitafanya kazi ya kudhibiti kabla ruhuka hajaingia ndani
ya punje (majuma 16 kabla ya kuvuna).
#15: Buu hubadilika kuwa mdudu kamili baada ya miezi 2 - 4 akiwa
ndani ya shina / mti. Mvua zinapoanza mdudu kamili (Mbawa kavu wa
bungua mweupe) hutafuna shina na kutengeneza tundu kubwa 8 mm la
mviringo la kutokea nje na kuanza tena mzunguko wa maisha.
#16: Kudhibiti Bungua Mweupe
1. Ngoa na choma mibuni iliyoshambuliwa sana.
20 TANZANIAN-GERMAN IPM PROJECT
2. Baada ya mavuno kwangua / sugua mashina ya kahawa kuondoa
magamba kwa gunzi ili kuondoa mayai na maeneo ya kutaga.
3. Kagua shamba na kukusanya mbawa kavu wa bungua weupe na
kuwaua. (kuanzia mwezi Oktoba, Novemba, Disemba, Januari).
4. Ua bungua weupe kwa kuwaondoa kwa waya (Oktoba / Novemba;
Aprili, Mei).
5. Weka mafuta ya wanyama kwenye matundu kuvutia sisimizi
watakao wala bungua.
6. Paka chokaa, udongo, majivu ili kukausha mayai yasianguliwe
kwenye shina na matawi. Changanya mkojo au mfori uliovundikwa
kwa siku 14 ili kuua au kufukuza wadudu.
7. Tumia madawa kama Mwarobaini, Utupa , Minyaa, Tumbaku au
sumu kama Decis 2% EC, Dursban 48%.
#20: Udhibiti:
Kilimo sango
Kuhimiza wadudu marafiki (manyigu, ladybirds)
Matumizi ya sumu ya asili:-
- Mkojo wa Ngombe 1:4
- Utupa gm 50 / lita ya maji
Kudhibiti sisimizi kwenye shina ili wasiwafikie vidungata.
Matumizi ya sumu za viwandani:-
- Inashauriwa kupaka shina la mti ulioadhirika sumu ili kuzuia
sisimizi wasiwafikie vidugamba.
- Shina lipakwe sumu ya Dursban kwa mchanganyiko wa mls 35
dawa kwenye kila lita moja ya maji.
- Sumu ipakwe urefu wa cm 15.
#24: Udhibiti:
Kilimo sango
Kuhimiza wadudu marafiki (manyigu, ladybirds)
Matumizi ya sumu ya asili:-
- Mkojo wa Ngombe 1:4
- Utupa gm 50 / lita ya maji
Kudhibiti sisimizi kwenye shina ili wasiwafikie vidungata.
Matumizi ya sumu za viwandani:-
- Inashauriwa kupaka shina la mti ulioadhirika sumu ili kuzuia
sisimizi wasiwafikie vidugamba.
- Shina lipakwe sumu ya Dursban kwa mchanganyiko wa mls 35
dawa kwenye kila lita moja ya maji.
- Sumu ipakwe urefu wa cm 15.
#25: Uharibifu na maisha yake
Mayai ya vithiripi hutagwa ndani ya majani ya kahawa na kwenye
magamba ya shina lake. Watoto wa vithiripi (Tunutu) wanaoanguliwa
huishi kwa kufyonza utomvu wa mmea kama vithiripi wapevu
wafanyavyo. Majani huanguka na hatimae mti mzima unaweza kufa.
Hatua ya buu hufanyikia ardhini ambapo mdudu mpevu hutokea na
kuendelea na uharibifu. Hali ya hewa ya ukame na joto humwezesha
mdudu huyu kustawi sana. Kizazi kimoja kinaweza kukamilika kwa
kipindi cha wiki 3.
#26: Uharibifu na maisha yake
Mayai ya vithiripi hutagwa ndani ya majani ya kahawa na kwenye
magamba ya shina lake. Watoto wa vithiripi (Tunutu) wanaoanguliwa
huishi kwa kufyonza utomvu wa mmea kama vithiripi wapevu
wafanyavyo. Majani huanguka na hatimae mti mzima unaweza kufa.
Hatua ya buu hufanyikia ardhini ambapo mdudu mpevu hutokea na
kuendelea na uharibifu. Hali ya hewa ya ukame na joto humwezesha
mdudu huyu kustawi sana. Kizazi kimoja kinaweza kukamilika kwa
kipindi cha wiki 3.